SERIKALI imepokea msaada wa Sh milioni 30 kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya kununua tiketi za mashabiki pamoja na motisha kwa wachezaji wa timu ya Tanzania (Taifa Stars).
Tanzania itacheza robo fainali ya CHAN dhidi ya Morocco, Agosti 22, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam leo wakati wa makabidhiano hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, aliishukuru benki hiyo kwa mchango huo akisema ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza michezo nchini.

