Na Mudy Kazi
INDIA: MWANAMUZIKI Surveen Chawla ameshangaza mashabiki na wadau wa filamu baada ya kudai kwamba alitakiwa awe na uzito mkubwa ndipo apewe nafasi ya kucheza katika filamu za kusini mwa India.
“Niliambiwa mimi ni mwembamba sana, sitaweza kuigiza katika filamu za Kusini mwa India.' Surveen Chawla ameeleza hilo kuwa ni changamoto kubwa nay a kushangaza aliyowahi kukutana nayo.
Muigizaji Surveen Chawla alianza safari yake ya uigizaji na vipindi vya televisheni kama vile ‘Kahin To Hoga na Kaajjal’, na baadaye akatambulika kwa uigizaji wake katika sinema ya Kipunjabi na Kihindi.
