NGULI katika filamu za mapigano Denzel Washington ameweka wazi kwamba afikilii kushinda Oscar nyingine kwa sababu tayari anazo mbili nyumbani kwake.

Muigizaji huyo wa Hollywood mwenye umri wa miaka 70 amepokea uteuzi wa Tuzo 10 za Academy kwa miaka iliyopita na ameshinda mara mbili, akitwaa tuzo ya Muigizaji Bora Msaidizi kwa tamthilia ya ‘Glory’ ya 1989 na kisha kutwaa Oscar ya Muigizaji Bora wa Siku ya Mafunzo ya 2001 lakini Denzel amekiri kuwa hafanyi chochote kumuwezesha kushinda tuzo hiyo.