KIPINDI cha kwanza cha Fainali kati ya Simba na Singida Black Stars kimekamilika huku Singida Black Stars wakiwa mbele kwa mabao mawili bila.
Goli la kwanza limefungwa na Jonathan Sowa baada ya kumzidi ujanja beki wa Simba na kupiga shuti kali kushoto kwa kipa Camara aliyebaki akiliangalia likiingia golini kwake.
Dakika chache baadae Camara aliumia baada ya kugongana na Jonathan Sowa katika harakati za kuokoa mpira wa juu. Baada ya kuumia alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na kipa wa Taifa Stars Ali Salim.
Uzembe wa kipa Ali Salim baada ya kuzembea kuupiga mpira akiwa ametoka eneo la goli aliposhindwa kupiga vyema mpira huo ukamkuta Emmanuel Kwame akalenga goli kwa guu lake la kushoto akafunga.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza Singida inaongoza kwa bao 2-0 dhidi ya Simba.
