RAIS wa Kenya William Ruto ametangaza siku saba za maombolezo nchini Kenya kutokana na kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Raila Odinga aliyefariki dunia leo nchini India kutokana na mshutuko wa moyo.
Katika kipindi hiki, bendera zote za Kenya zitapepea nusu mlingoti kama ishara ya heshima na maombolezo.
Hospitali ya Devamatha katika jimbo la Kerala imethibitisha taarifa za kifo chake leo. Odinga amefariki akiwa na miaka 80, aliwahi kugombea urais wa Kenya mara tano katika kipindi cha zaidi ya miongo mitatu.
Mwezi machi, Raila Odinga alikuwa amesaini makubaliano ya kisiasa na
rais William Ruto ambayo yalikiruhusu chama chake cha upinzani cha ODM
kushiriki katika mchakato muhimu wa kupitisha sera huku baadhi ya wanachama
wake wakiteuliwa kuwa mawaziri.
Viongozi mbalimbali duniani wameanza kutuma salamu za rambirambi akiwemo
rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

